Jumatatu 3 Agosti 2026 - 07:45
Shambulio dhidi ya Misri ni sehemu ya mpango wenye sumu wa Marekani wa kuchochea fitna katika eneo

Hawza/ Abdul Bari Atwan, mchambuzi mashuhuri wa ulimwengu wa Kiarabu, amesema kuwa; shambulio la ndege zisizo na rubani dhidi ya Bandari ya Damietta nchini Misri ni sehemu ya mpango uliobuniwa mjini Washington, unaolenga kuiingiza Misri katika migogoro ya kikanda, kuchochea fitna za kimadhehebu na kufidia kushindwa kwa Marekani na utawala wa Kizayuni katika eneo.

Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, kikinukuu Islami Analysis, Abdul Bari Atwan, akirejelea shambulio la ndege zisizo na rubani dhidi ya meli moja ya Marekani na meli moja ya Ugiriki katika Bandari ya Damietta nchini Misri, alieleza kuwa tukio hilo ni sehemu ya mpango uliopangwa mapema kwa lengo la kuleta hali ya kuyumba usalama nchini Misri.

Akibainisha kuwa Misri katika miaka ya hivi karibuni imejiepusha na migogoro ya kikanda na badala yake imejikita katika kujenga upya uwezo wake wa kijeshi, kiuchumi na nafasi yake ya kikanda, alisema: "Kwamba sasa Misri imekuwa habari kuu katika eneo si jambo la bahati mbaya. Hakuna mwingine aliye nyuma ya njama hii dhidi ya Misri isipokuwa utawala wa Kizayuni." Kwa mujibu wa Atwan, mpango huo ulitayarishwa mjini Washington.

Mchambuzi huyo wa Kipalestina, akirejelea ukimya wa Tel Aviv kuhusu shambulio hilo, alidai kuwa mpango wa operesheni hiyo uliandaliwa wakati wa ziara ya hivi karibuni ya Benjamin Netanyahu nchini Marekani na mkutano wake na Donald Trump katika Ikulu ya White House.

Alisema: "Shambulio dhidi ya Bandari ya Damietta ni moja ya matokeo ya mpango wenye sumu, wa njama na wa fitna ambao Netanyahu aliuwasilisha katika mkutano wake na Trump."

Kupinga kwa Misri gesi ya Israel

Atwan alisema kuwa; sababu nyingine ya hatua hiyo ni juhudi za Misri za kupunguza utegemezi wake wa gesi ya utawala wa Kizayuni. Alisema Cairo inatafuta kupanua vyanzo vyake vya nishati, jambo ambalo kwa mujibu wake halikubaliki kwa Tel Aviv na linaonekana kuwa ni kutoka katika utegemezi wa kiuchumi ambao Israel inautaka kwa Misri.

Juhudi za kuchochea vita vya kimadhehebu

Akirejelea kushindwa kwa Marekani na utawala wa Kizayuni kufanikisha malengo yao dhidi ya Iran, Atwan alidai kuwa Washington na Tel Aviv sasa zinajaribu kufufua mradi wao wa zamani wa kuchochea migogoro ya kimadhehebu katika eneo.

Atwan alisema: "Walishindwa vitani, hawakuweza kuilazimisha Iran kujisalimisha, na sasa kwa mara nyingine wanatafuta kuzusha fitna kati ya Ahlu Sunna na Mashia ili kulitumbukiza eneo katika machafuko."

Msaada wa wananchi wa Misri kwa Mhimili wa Muqawama

Mchambuzi huyo pia aliongeza kuwa; sehemu kubwa ya wananchi wa Misri wana mtazamo chanya kuhusu Iran na wanaunga mkono Mhimili wa Muqawama; jambo ambalo limezua wasiwasi kwa Marekani, utawala wa Kizayuni na baadhi ya serikali za Kiarabu.

Atwan pia alipinga kuhusishwa kwa shambulio hilo na Harakati ya Ansarullah ya Yemen, akisema kuwa; madai hayo ni sehemu ya operesheni ya vyombo vya habari. Akirejelea uhusiano wa kihistoria kati ya Misri na Yemen, alisema: "Wayemeni hawakuchukua hatua yoyote dhidi ya Misri hata wakati ambapo nchi hiyo ilipata hasara ya mabilioni ya dola kutokana na kupungua kwa idadi ya meli zilizokuwa zikipita katika Mfereji wa Suez. Licha ya kuwepo kwa zaidi ya Wayemeni milioni mbili nchini Misri, hakuna mantiki yoyote ya kuamini kwamba wangependa kwa kushambulia Bandari ya Damietta wawe chanzo cha fitna."

Katika sehemu nyingine ya mazungumzo yake, Atwan pia alitathmini maendeleo ya hivi karibuni yanayohusiana na Ukraine kuwa ni sehemu ya mpango huohuo. Akirejelea tangazo la serikali ya Iraq kuhusu kukamatwa kwa kundi la wahujumu uchumi linalohusishwa na Ukraine, alisema kuwa; shughuli za Kyiv nchini Iraq pamoja na shambulio dhidi ya shabaha moja ya Iran katika eneo la Bahari ya Caspian zinaonesha kuwepo kwa mpango ulioratibiwa.

Mwishoni, Atwan alidai: "Jumla ya matukio haya yanaonesha kuwa kuna njama ya Kizayuni inayoungwa mkono na Marekani kwa lengo la kuficha kushindwa kwa nchi hiyo nchini Iran, katika Mlango wa Hormuz na katika maeneo mengine ya eneo hili."

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha